Showing posts with label ya. Show all posts
Showing posts with label ya. Show all posts
Tuesday, April 18, 2017
MAGONJWA YA UTANDO MWEUPE KINYWANI
MAGONJWA YA UTANDO MWEUPE KINYWANI

ziko sababu nyingi zinazoweza kusababisha hali hii ya kutokea kwenye kinywa, lakini chanzo chake kikubwa ni maradhi yanayosababishwa na fangasi.
Utando wa kinywa ni maradhi ni maradhi yanayosababishwa na vimelea vya fangasi aina ya hamira ambao hushambulia eneo la ndani ya kinywa na koo.
Kwa kawaida kinga ya mwili pamoja na vimelea vinavyokaa mwilini vya aina ya bacteria huzuia fangasi hawa wasiongezeke.

Inapotokea uwiano huu wa kinga ya mwili na vimelea aina ya bacteria kushindwa kuzuia ongezeko la vimelea hivyo vya fangasi ndipo hali huwa mbaya na kusababisha utando mdomoni.
Maradhi haya ni kawaida kuonekana kwa watoto wachanga. Maradhi haya hutokea kutokana na hali ya kutokuwa na uwiano sahihi kati ya kinga ya mwili wa mtoto na vimelea aina ya bacteria.

Inapotokea yakatokea kwa mtu mzima, basi mara nyingi huwa kuna viashiria hatarishi kama vile upungufu wa kinga.
Mfano ni watu wenye maradhi ya muda mrefu kama saratani, kisukari na ukimwi au mwanamke wajawazito, hali hiyo hushusha kinga zao.
Tatizo hili huwapata pia watu wanaotumia dawa kwa muda mrefu hususani dawa za vijiuasumu (antibiotic) au za maradhi yanayotibiwa kwa muda mrefu kama vile saratani.
Kinachoweza kusababisha hali hiyo pia ni msongo wa mawazo wa muda mrefu.

Maradhi haya kwa kawaida siyo ya kuambukiza ingawa mtoto mchanga mwenye maradhi haya huweza kuyaambukiza matiti ya mama yake.
Dalili ni utando mweupe ambao huonekana kwenye kinywa eneo la ulimi na mashavuni kwa ndani. Kwenye koo huonekana kwenye kuta zake.
Mara nyingi eneo lenye rangi nyeupe huzungukwa na eneo lenye rangi nyekundu na lililovimba kidogo. Hii hutokana na mashambulizi ya fangasi.
Maeneo haya yaliyoshambuliwa huwa hayana maumivu makali lakini huweza kutoa damu kama yakiguswa au kusuguliwa.
Dalili nyingine za maradhi ni pamoja na kuonekana kwa sehemu ndogo zenye rangi nyeupe ndani ya kinywa, kupasuka kwa midomo, midomo kuongezeka ukubwa, hisia za kukwama kwa chakula kwenye koo, kuvimba kwa fizi, ladha ya chakula kubadilika na pumzi yenye kutoa harufu.

Kwa watu ambao kinga kinga ya mwili imeshuka, maradhi haya huweza kusambaa kutoka kwenye kinywa na kushuka kwenye koo la chakula mpaka kufikia kwenye tumbo.
Hii inapotokea, mgonjwa hupata maumivu wakati wa kumeza chakula.
Dalili za hatari ni mgonjwa kupata homa kali ikiambataan na kutetemeka mwili na kushindwa kabisa kumeza chakula.
Mgonjwa akifikishwa hospitali maradhi haya hutambulika kirahisi kutokana na dalili zake kuweza kutambukiwa kwa kuangalia kwa macho.
Matibabu ya maradhi haya hutegemea na kilichosababishwa. Iwapo kilichosababisha kinaweza kuepukwa au kutibika, basi nayo yataisha, kama mtu ameyapata kutokana na kuugua kisukari, ni vyema akakitubu kisukari kwanza.
Watoto wachanga hawahitaji matibabu ya aina yeyote kama dalili zitaanza kuisha kabla ya wiki nne hazijaisha.


Tiba Mbadala Ya Fangasi Kwenye Ulimi tumia Dawa Hii Hapa:
Kula Kitunguu Saumu kibichi kutwa mara 3 kwa muda wa siku 7 utapona , Pendelea kunywa Mtindi pia utasaidia hayo matatizo ya Fangasi ya mdomo. Tafuta Mafuta yanayoitwa Oregano Oil uwe unatia kwenye glasi ya maji kijiko kidogo au kijiko cha kulia wali unakunywa kutwa mara 3 kwa muda wa siku 3 utapona inshallah hiyo Fangasi kwenye ulimi.
Available link for download
Sunday, April 16, 2017
Main Rahoon Ya Na Rahoon Full Video Emraan Hashmi Esha Gupta Amaal Mallik Armaan Malik
Main Rahoon Ya Na Rahoon Full Video Emraan Hashmi Esha Gupta Amaal Mallik Armaan Malik
Available link for download
Tuesday, February 28, 2017
MARADHI 27 YANAYOTIBIWA KWA KUTUMIA ASALI YA NYUKI
MARADHI 27 YANAYOTIBIWA KWA KUTUMIA ASALI YA NYUKI

Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote.Vitabu vingi vya zamani vinazungumzia namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali.Moja ya vitabu hivyo ni KURUANI TUKUFU ambayo Mwenyezi Mungu
anaitaja asali kama tiba(AN-NAHL 16:68-69).Sasa hivi kuna makala nyingi zilizo andikwa zikielezea kuhusu uwezo wa asali katika tiba ya magonjwa mbalimbali.Warusi na Wafaransa wanafahamika sana katika kufanya utafiti katika maabara kuhusu uwezo wa asali katika tiba mbali na Kuruani Tukufu kuna
baadhi ya vitabu vingine vinavyofahamika kuandikwa na watafiti kuhusu uwezo wa asali katika tiba.Moja kile cha BEES DONT GET ARTHRITIS CHA FRED MALONE NA BEE IN BALANCE CHA AMBER ROSE.
Leo tuangalie tiba ya asali na mdalasini na namna ya kuitumia kutibu maradhi mbalimbali(asali tunayoizungumzia hapa ni asali safi mbichi.)
BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA KWA ASALI NA MDALASINI NI KAMA IFUATAVYO:
1.UGONJWA WA VIUNGO/MAUMIVU NA UVIMBE(ARTHRITIS)
-Chukua maji kiasi vuguvugu na ongeza mdalasini (unga kijiko cha chai na asali vijiko 2 vya chakula na kuchua sehemu zenye maumivu)
-Vilevile waweza kutengeneza kikombe kimoja cha chai kwa kuweka kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na kuongeza asali vijiko viwili vya chakula na kisha kunywa ikiwa ya moto kutwa mara mbili(asubuhi na jioni)
2.KUKATIKA KWA NYWELE(HAIR LOSS)
-Asali ikichanganywa na mdalasini na mafuta vuguvugu ya olive hutia kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele.
-Tumia mchanganyiko huo vuguvugu kwa kupaka na kusugua kichwani na acha kwa dk 15 kisha uoshe.
3.UKUNGU WA MIGUU(FUNGUS)
-Changanya kijiko cha chakula cha asali na vijiko viwili vya chai vya mdalasini na acha kwa muda wa nusu saa kisha safisha .(rudia hivyo mpaka upone)
4.MAAMBUKIZI KWENYE KIBOFU CHA MKOJO(BLADDER INFECTION)
-Changanya maggy ya maji vuguvugu na vijiko2 vya chai vya mdalasini na kijiko1 cha asali huondoa bakteria kwenye kibofu.
5.MAUMIVU YA JINO(TOOTHACHE)
-Changanya sehemu tano za asali na sehemu moja ya mdalasini na dondoshea kwenye jino linalouma hadi maumivu yatakapotoweka.
6.VIDONDA VITOKANAVYO NA MAGONJWA YA KULALA KWA MUDA MREFU(BED SORES)
-Paka saladi iliyochanganywa asali na mdalasini.Vilevile tumia chai ya roseberry nyekundu kwa kuondoa maumivu makali ya canker sores/bed sores.
7.LEHEMU(CHOLESTRAL)
-Changanya asali safi mbichi vijiko2 vya chakula na unga wa mdalasini vijiko2 vya chakula na kikombe cha chai cha maji ya moto na unywe kutwa mara 3
8.MAFUA(COLDS)
-Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali vuguvgugu na robo kijiko cha unga wa mdalasini kuondoa chafya na kuvimba koo.
9.UGUMBA(INFERTILITY)
-Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi.Kwa wapenzi. wa jinsia zote wanashauriwa kunywa walau vijiko 2 vya chakula kila siku kabla ya muda wa kulala..Mdalasini imetumika muda mrefu katika dawa za kichina na kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa
-Changanya mdalasini na kiasi cha asali na kufanya mgando (paste)na upake kwenye fizi na meno na kuacha inyonywe na kuingia mwilini taratibu na hii ni kwa akina mama wasio na sababu za kimsingi za kuwakosesha kuzaa.
10.MCHAFUKO WA TUMBO(STOMACH UPSET)
-Asali kwa muda mrefu imetambulika kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo na kichefuchefu.Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali pia hupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
11.GESI(ACID)
-Kula asali pamoja na mdalasini kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi(acid)huu ni uchunguzi ulio fanywa na Japan na India
12.UGONJWA WA MOYO(HEART DISEASE)
-Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara kwa kupakaa kama jam wakati wa kula mkate wa ngano wenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko 1 cha chakula cha mchanganyiko huo(asali na mdalasini) kila siku
13.SHINIKIZO LA DAMU(H/B/P)
-Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya upata dozi ya mara kwa mara ya asali iliyochanganywa na mdalasini.
14.KINGA YA MWILI(IMMUNE SYSTEM)
-Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja.Utafiti unaonyesha kuwa hazina kubwa ya vitamini(virutubisho),madini pamoja na mchanganyiko wa mdalasini na asali iondoayo magonjwa na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za damu husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea(virus)na bakteria.
15.UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME(UHANITHI/IMPOTENCE)
-Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu ya uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji.Asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za mashariki za dunia.Watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali inauwezo wa kupelekea mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo mdalasini.
-Katika Afrika na dunia ya kusini mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi.
16.KUTOKUCHAGULIWA KWA CHAKULA(INDIGESTION)
-Kula vijiko 2 vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo huondoa kiungulia na wataalam wanasema asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa chakula tumboni na mdalasini unaongeza kasi ya kuchaguliwa kwa chakula.
17.FLU(INFLUENZA)
-Tafiti moja ya Kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa iliyopo katika asali ni dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu vimelea(virus)waletao flu.
18.KUONGEZA UMRI WA KUISHI(LONGEVITY)
-Unaweza kuishi hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali.Kutengeneza kinywaji hiki kitamu weka vijiko
4(vikubwa)vya mdalasini na vijiko 4 vya asali,vikombe 3 vya maji na koroga kwa dk 10 kisha kunywa robo kikombe mara 3 au 4 na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.
19.KUONDOA CHUNUSI(PIMPLES)
-Changanya vijiko 3 vikubwa vya asali na kijiko 1 kikubwa cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.Uwezo wa asali wa kuua bakteria unafanya uso kuwa wa kawaida katika muda wa wiki 2.
20.KUUMWA NA WADUDU(WASHA WASHA WENYE SUMU)
-Changanya asali na mdalasini kisha pakaa moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia tena hadi uvimbe uishe.
21.MADHARA YA NGOZI(INFECTIONS)
-Fanya kama ilivyoandikwa namba ishirini hapo juu.
22.KUPUNGUZA UZITO.
-Waweza kufurahia vyakula vyote unavyovipenda kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri kilichojaa vitu muhimu viwili ambavyo ni asali na mdalasini.
-Unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako.Vilevile wataalam wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyama nyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko 2 vikubwa vya asali na kijiko 1 cha mdalasini.Rudia mchanganyiko huo kabla ya kulala.Wataalam wamethibitisha kuwa inapunguza hamu ya kula na kuleta joto mwilini.
23.SARATANI(CANCER)
-Utafiti uliofanyika huko Australia na Japan umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya magonjwa kwa anaetumia madawa ya kutibu saratani.Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua saratani ya mifupa na utumbo ambao walikuwa wanatumia kila siku dozi ya asali na mdalasini walionyesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wanatumia madawa ya kutibu saratani peke yake.Dr.HIROKI OWATA alisema waliwapa mchanganyiko wa asali na mdalasini kijiko kimoja kutwa mara 3 kwa mwezi 1 na wengine waliendelea kama kawaida.
24.KUONDOA UCHOVU(FATIQUE)
-Uko ushahidi kwamba sukari asilia iliyopo katika asali inauwezo wa kuongeza nishati mwilini.Zikitumika ipasavyo sukari hii inaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.Wataalam wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu kikombe cha maji yaliyonyunyiziwa mdalasini kunywewa masaa mawili baada ya kuamka.Rudia kunywa saa 9 alasiri wakati nishati(nguvu)inapoanza kuisha kufuatia ushauri wa dr.MILSTON ABBOZZA ambaye kazi zake kuhusu asali na
Read more »
Available link for download
Subscribe to:
Posts (Atom)